Wachezaji wa Nigeria wakishangilia ubingwa wao. |
Mwananchi, Jumatatu,Februari11 2013
NIGERIA ilitawala mchezo wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kuifunga Burkina Faso bao 1-0 na kutwaa taji mjini, Johannesburg, Afrika Kusini.
Sunday Mba alikuwa shujaa wa ushindi wa Nigeria
(Super Eagles) baada ya kufunga bao pekee dakika tano kabla ya filimbi
ya kutenganisha nusu ya mchezo huo mkali ulioshuhudiwa na watazamaji
85,000.
Wilfried Sanou angeweza kusawazisha bao hilo kwa
Burkina Faso (Stallions) katikati ya kipindi cha pili, shukrani kwa kipa
wa Nigeria Vincent Enyeama aliyecheza vizuri kuokoa hatari hiyo.
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Nigeria hatua ya fainali tangu mwaka 2000, na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji mbele ya Burkina Faso, taifa dogo Afrika Magharibi.
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Nigeria hatua ya fainali tangu mwaka 2000, na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji mbele ya Burkina Faso, taifa dogo Afrika Magharibi.
Burkina Faso haijawahi kuifunga Nigeria katika
mechi 12 walizokutana katika mashindano mbalimbali, na hiyo ilitosha
kuipa Nigeria nafasi ya kushinda mchezo. Efe Ambrose alikuwa na nafasi
tano za kufunga kipindi cha kwanza, lakini ya kukumbukwa zaidi ni pale
alipopiga juu mpira akimalizia kiki ya adhabu ndogo kutoka kwa Victor
Moses ndani ya dakika saba tangu kuanza mchezo.
Nigeria waliotawala mchezo kwa kiasi kikubwa,
walikaribia kufungwa kama siyo, Aristide Bance kupoteza nafasi nzuri ya
kufunga baada ya shuti lake la mita 25 kukosea shabaha na kwenda nje ya
lango huku.
Nigeria wangeweza kufunga bao la pili kama Ideye
angetumia vizuri pasi aliyopewa kuusindikiza kirahisi mpira wavuni,
lakini akaishia kupiga nje.
Huo ni ubingwa wa tatu kwa Nigeria, lakini wa
kwanza kwa tangu mwaka 1994 walipotwaa mara ya mwisho baada ya kuifunga
Zambia mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.
REKODI
Nigeria:
Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi anakuwa kocha wa pili kama mchezaji kutwaa taji na pia kama kocha katika historia ya michuano hiyo, akiungana na Mahmoud Al Gohari wa Misri.
Nigeria ina rekodi ya pekee ya kiwango cha ubora
wa soka duniani (Fifa), kwani ndiyo timu pekee Afrika iliyowahi kushika
nafasi ya tano duniani mwaka 1994. Kwa sasa inashika nafasi ya 52.Kwa
mara ya kwanza Nigeria ilicheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994,
ikiwa kundi moja na Bulgaria, Ugiriki na Argentina na kufanikiwa
kuongoza kundi lake.
Iliifunga Bulgaria 3ñ0, ikapoteza kwa kufungwa
mabao 2-1 na Argentina na kufanikiwa kusonga mbele raundi ya pili baada
ya kuifunga Ugiriki mabao 2ñ0.
Katika raundi ya pili, Nigeria ilicheza na Italia,
ambapo mpaka dakika 25 za kwanza tayari walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0
lililofungwa na Emmanuel Amunike.
Burkina Faso:
Kwa upande wa Burkana Faso, haina rekodi nyingi na nzuri za mafanikio katika soka la kimataifa kama ilivyo kwa Nigeria. Awali, Burkina Faso ilikuwa ikijulikana kama Upper Volta mpaka mwaka 1984, ilipobadilika jina na kuwa la sasa. Waliandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
mwaka 1998 na kumaliza katika nafasi ya nne, lakini mafanikio makubwa
waliyopata ni kufika hatua ya fainali mwaka huu.
No comments:
Post a Comment