Tuesday, February 12, 2013

Wanakwenda wapi wakifeli kidato cha nne?





Mwananchi, Jumanne, Februari5  2013

MWAKA 2011, nchi ilishuhudia idadi kubwa ya wanafunzi wakifeli mtihani wa kidato cha nne kwa kupata daraja sifuri.Kwa mujibu wa kumbukumbu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, watahiniwa 156,089  sawa na asilimia 46.41ya wahitimu wote walifeli mtihani huo kwa kupata daraja hilo la mwisho.Katika mtihani huo wanafunzi 33,577 pekee sawa na asilimia 9.98 ndio waliopata kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu, hivyo kuwa na uhakika wa kuendelea na kidato cha tano.

Kwa mujibu wa mfumo wa elimu nchini, wanaopata daraja la nne, baadhi wako shakani kuendelea na daraja la sekondari ya juu. Katika matokeo hayo, hawa walikuwa 146,639 sawa na asilimia 43.60.Ili kujiunga na kidato cha tano, wanafunzi hawa wanapaswa kuwa na alama C katika masomo yasiyopungua matatu.
Aidha, kwa waliopata daraja sifuri ni sawa na kusema miaka minne ya kuwa shule, wameambulia patupu, kwani kwa mfumo uliopo wa elimu hawawezi kuendelea kusoma, labda warudie mitihani au wajiunge na vyuo vinavyopokea wahitimu wa darasa la saba.
Bila shaka jeshi hili la vijana waliofeli ni kubwa, na kwa kuwa nchi haina utaratibu wa kuwaendeleza, swali kuu ni je, wahitimu hawa wanakwenda wapi, wana sifa ya kuajiriwa au hata kuwa na uwezo wa kujiajiri? Kwa habari zaidi bofya hapa.

Nigeria mabingwa Afcon 2013

Wachezaji wa Nigeria wakishangilia ubingwa wao.


Mwananchi, Jumatatu,Februari11  2013

NIGERIA ilitawala mchezo wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kuifunga Burkina Faso bao 1-0 na kutwaa taji mjini, Johannesburg, Afrika Kusini.
Sunday Mba alikuwa shujaa wa ushindi wa Nigeria (Super Eagles) baada ya kufunga bao pekee dakika tano kabla ya filimbi ya kutenganisha nusu ya mchezo huo mkali ulioshuhudiwa na watazamaji 85,000.
Wilfried Sanou angeweza kusawazisha bao hilo kwa Burkina Faso (Stallions) katikati ya kipindi cha pili, shukrani kwa kipa wa Nigeria Vincent Enyeama aliyecheza vizuri kuokoa hatari hiyo.
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Nigeria hatua ya fainali tangu mwaka 2000, na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji mbele ya Burkina Faso, taifa dogo Afrika Magharibi.
Burkina Faso haijawahi kuifunga Nigeria katika mechi 12 walizokutana katika mashindano mbalimbali, na hiyo ilitosha kuipa Nigeria nafasi ya kushinda mchezo. Efe Ambrose alikuwa na nafasi tano za kufunga kipindi cha kwanza, lakini ya kukumbukwa zaidi ni pale alipopiga juu mpira akimalizia kiki ya adhabu ndogo kutoka kwa Victor Moses ndani ya dakika saba tangu kuanza mchezo.
Nigeria waliotawala mchezo kwa kiasi kikubwa, walikaribia kufungwa kama siyo, Aristide Bance kupoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya shuti lake la mita 25 kukosea shabaha na kwenda nje ya lango huku.
Nigeria wangeweza kufunga bao la pili kama Ideye angetumia vizuri pasi aliyopewa kuusindikiza kirahisi mpira wavuni, lakini akaishia kupiga nje.
Huo ni ubingwa wa tatu kwa Nigeria, lakini wa kwanza kwa tangu mwaka 1994 walipotwaa mara ya mwisho baada ya kuifunga Zambia mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.


Rais Kikwete amjibu Lowassa tatizo la ajira nchini







Na Tausi Mbowe na Habel Chidawali, Dodoma
Posted  Jumatatu,Februari11  2013  saa 24:44 AM
Mwananchi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete katika hali inayoashiria kumjibu rafiki yake, Edward Lowassa ameponda makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua semina ya siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma jana, alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo hakuna maana ikiwa mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo hilo.
Ingawa hakutaja majina ya wanasiasa ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo lakini Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la ajira kwa maneno kwamba ‘ni bomu linalosubiri kulipuka’. Kwa habari zaidi boya Hapa.

Wednesday, February 6, 2013

Vyuo vya ufundi stadi kichocheo muhimu cha maendeleo ya Taifa





Na Fred Ayazi, Mwananchi. February 5 2013

KILA mwaka, zaidi ya nusu ya wanafunzi wanaohitimu darasa la saba na kidato cha nne, hawapati fursa ya kuendelea na ngazi ya elimu iliyo mbele yao kwa sababu mbalimbali.
Mfano mzuri ni mwaka jana ambapo wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba walikuwa 983, 545, lakini waliofaulu ni 567,567. Hivyo wanafunzi 415,978 hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari.
Katika kundi hili wamo watakaosomeshwa na wazazi, walezi ama wafadhili katika shule binafsi. Lakini kuna maelefu wengine watakwama kabisa kuendelea na elimu ya sekondari.
Kwa nchi masikini kama Tanzania, kuzalisha watu zaidi ya 500,000 kila mwaka ambao hawapati ujuzi wowote, ni kuongeza umaskini katika nchi ambayo hivi karibuni tulielezwa kuwa idadi ya watu wake imefika milioni 44.