Tarehe:25 Oktoba 2024
Katika kuendeleza dhamira yetu ya kuwawezesha watoto kupitia michezo na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii, YOSSO (Youth Social Sports Organization) imetoa msaada wa mpira wa miguu na mpira wa mikono kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mavurunza.
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa YOSSO, Prosper Mambo, aliongoza tukio hilo kwa kukabidhi mipira hiyo kwa shule kwa ajili ya kuwawezesha watoto wa kike na wa kiume kushiriki michezo. Mradi huu unalenga kuhamasisha watoto kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao, kuimarisha afya yao, na kuwajengea uwezo wa kijamii.
Tunatoa shukrani kwa wanachama wote na wadau wanaoendelea kuunga mkono jitihada za YOSSO katika kuboresha maisha ya vijana na jamii kwa ujumla kupitia michezo. Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za miradi na shughuli nyingine zinazofanywa na YOSSO kupitia blogu hii.
#YOSSO #MichezoKwaMaendeleo #EmpowermentThroughSports #MavurunzaPrimary